Kili MusicTour 2013

Kili Tour kwa mwaka 2013 lilikuijia likiwa na kauli mbiu ya “Kikwetu kwetu” kwani burudani iliyokuwa ikitolewa ni kutoka kwa wasanii wa nyumbani, wakikupa ladha za ala za muziki wa nyumbani na katika viwanja vya nyumbani.

Shangwe tupu zilitawala kwenye kila kiwanja kilichofanya tamasha la Kili Music Tour 2013.

Wasanii mbalimbali waliweza kuweka historia kwenye hili tamasha kubwa hapa nchini kwetu Tanzania. Vipaji tofauti viliweza kuonekana na hata shangwe za mashabiki wao.

Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Fleva), Nassib Abdul a.k.a Diamond, Ali Kiba, Lady Jay dee, Roma Mkatoliki, Kala Jeremiah na wengine wengi waliweza kutoa burudani ya nguvu iliyokonga nyoyo za mashabiki katika mikoa mbalimbali ambayo Kili Musci Tour iliweza kufika na kutoa burudani.