Jumatatu , 28th Nov , 2022

Uongozi wa soko la baba na mama lishe Kisutu jijini Dar Es Salaam wamesema serikali iwashughulikie kundi la mama lishe na baba lishe ambao wanaondoka sokoni hapo na kurejea mitaani kwa kigezo cha kushindwa kulipa ushuru wa shilingi mia tano.

Akizungumza nasi katibu wa soko hilo Bakari Hussein amesema utaratibu uliopo kwa sasa baada serikali ya mkoa kuwahamishia katika soko hilo kuna baadhi yao wameanza kurejea mitaani na kupika chakula katika maeneo yaliyokatazwa na kukiuza kwa bei chini hali inayoleta upinzania kibiashara.

Wamesema kwa siku utaratibu kwa kila mfanyabiashara anatakiwa kulipa shilingi mia tano kupitia control namba maalum hivyo kurejea kwa mitaani kunapoteza mapato ya jiji lakini pia kuwaumiza wengine wanalipa ushuru huo.

Kwa upande wao mama lishe na baba lishe hao wamesema biashara sokoni hapo inabadilika kulinga na siku wakiiomba serikali ya mkoa kudhibiti wote walioko mitaani ili kurejesha utulivu wa kibiashara.