Ijumaa , 6th Jan , 2023

Wafanyabiashara wa mawe ya urembo na nakshi za majengo maarufu kama Tanga stone wameiomba Serikali kuwawezesha kimitaji kwa kuwapatia tenda mbalimbali za ujenzi kwenye miradi ya kiserikali ili kupata fursa ya kukuza mitaji na kujiinua kiuchumi.

Kwa takribani miaka 25 kijana aliyejitambulisha kwa jina la Abbas Abdalah amekuwa akijihusisha na uuzaji wa mawe ya urembo ambayo huyafata jijini Tanga na kuyaleta hapa jijini Dar es Salaam kisha kuyauza kwa matumizi mbalimbali ameeleza changangamoto za kibiashara anazokutana nazo ikiwemo udogo wa mtaji licha ya kupata oda kubwa za wateja ambazo hana

Amesema licha ya Serikali kutoa mikopo kwa baadhi ya makundi ya vijana yeye amekuwa akichengana na fedha hizo na hajawahi kuzipata hivyo sasa kuomba serikali iwatambue vijana wenye uwezo na mawazo kupata sehemu kwenye miradi ya kisekta ili kuwakuza kibiashara.

Pamoja na ugumu anaopitia katika biashara zake wapo vijana ambao amekuwa akiwashirikisha pindi anapopata tenda kubwa za wateja hivyo kuwa sehemu ya kipato chao

Tanzania inatajwa kuwa na rasilimali nyingi za asili ikiwemo Mawe haya ambayo huchimbwa ardhini yakiwa na uwezo wakutumiwa katika majengo tofauti tofauti.