Ijumaa , 21st Jun , 2019

Mzee wa miaka 70 amekamatwa nchini Uganda kwa tuhuma za kulipiga mawe gari ya Rais Museveni likiwa kwenye msafara mwaka jana.

Gari ya Rais iliyoshambuliwa

Mzee Omar Risasi Amabua alikamatwa katika Mji wa Arua na baadaye kuhamishiwa katika mahabusu iliyoko Gulu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nile Magharibi, Christopher Barugahare mtuhumiwa huyo atashtakiwa kwa uhaini.

"Tumemkamata kwa sababu amehusishwa na tukio la mwaka jana ambapo gari la rais lilishambuliwa kwa mawe", amesema Barugahare.

Gari hilo lilishambuliwa Augosti 13, 2018, siku ya mwisho wa kapeini za uchaguzi mdogo wa Manispaa ya Arua.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia mauaji ya kinyama ya Mbunge Ibrahim Abiriga na mlizi wake ambaye alitajwa kuwa ndugu yake. Tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ameagiza vitengo vya usalama kuwatafuta wauaji wa kiongozi huyo.