Ijumaa , 20th Mei , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Songwe limemkamata Edward Simfukwe (45) Mkazi wa Kijiji cha Ikana Wilayani Momba akiwa na risasi 8 bila kuwa na bunduki ambapo baada ya kumbana amewataja watu wawili ambao huwa wanamuazima bunduki kwa ajili ya kufanya uhalifu

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Janeth Magomi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Janeth Magomi amesema Polisi pia wamekamata nyara mbalimbali za serikali ikiwa ni pamoja na Pembe moja ya mnyama aina ya pofu na mkia wake, Ngozi ya Duma, Pamoja na Ngozi ya Kenge sambaba na pikipiki 7 na vitu mbalimbali vya nyumbani.

Polisi wamewataka wamiliki wote wa silaha mkoani humo kuwa makini kuzitunza na kuepuka kuwaazima watu kwa ajili ya kufanya uhalifu