Ijumaa , 20th Jan , 2023

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Rama anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40  mkazi wa Morogoro amekutwa akiwa uchi ndani ya  kanisa la Anglikana lililopo mtaa wa Matema kata ya Maguvani Halmashauri ya mji wa Makambako

Katibu wa kanisa la Anglikani Makambako Elias Ngailo amethibitisha kukutwa kwa mtu huyo, na kueleza kuwa amekutwa akiwa mtupu na amelala, hivyo wamelazimika kumsaidia  kumvalisha nguo na kumpeleka kituo cha polisi wilaya ya kipolisi Makambako

Aidha katibu huyo amesema hajafahamu bado kama mtu huyo anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili na kueleza kuwa pindi matukio hayo yanapotokea jamii haipaswi kujichukulia sheria mkononi

Naye Mwinjilisti wa kanisa hilo John Kisogo amesema mara baada ya kumkuta mtu huyo katika madhabahu hiyo wamelazimika kumfanyia huduma ya maombi na kufanya naye mahojiano ambapo hajui amefikaje kanisani hapo.

Hata hivyo mtunza hazina wa kanisa hilo Christopher Mtweve amesema kuwa huenda mtu huyo akawa na matatizo ya akili