
Jaji Mstaafu Joseph Warioba
Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na taasisi mbalimbali za kupinga ukatili, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, amesema kuwa vurugu huingilia haki za binadamu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC,Anna Henga amewataka wanajamii kuacha kukaa kimya pindi vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unatokea.
Aidha, wamewataka wananchi wote kuilinda amani ya nchi kwani amani isipoimarika kutatokea vurugu na kushindwa kulinda haki za binadamu.