
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Gregory Mushi
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Gregory Mushi, na kusema mtuhumiwa huyo alitenda jinai hyo majira ya saa 11:00 alfajiri na baada ya kutenda tukio hilo alifanikiwa kukimbia akipewa msaada wa baba mzazi wa mtoto huyo na kukimbilia kusikojulikana.
Hata hivyo jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata baba mzazi wa mtoto huyo kwa kosa la kumtorosha mtu aliyemjeruhi mtoto wake.