Jumatano , 28th Dec , 2022

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA John Mrema, amesema kuwa endapo uchaguzi wa mwaka 2025 utakuwa huru na haki wanayo matarajio makubwa kwamba watashinda uchaguzi huo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA John Mrema,

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na EATV &EA Radio Digital, wakati akielezea matarajio yao kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

"Kwa hatua ya sasa tunapambana kutafuta Katiba Mpya, na Tume Huru ya Uchaguzi, ambayo itasimamia uchaguzi ulio huru na wa haki endapo vitu hivyo vikipatikana matarajio yetu ni makubwa na ni ya kushinda, na hivyo visipopatikana tutavuka mto," amesema Mrema.

Tazama video hapa chini