Jumatatu , 16th Jan , 2023

Mamlaka ya Afrika Kusini iko katika harakati za kumsaka chui anayemilikiwa na mtu binafsi ambaye ametoroka kutoka kwenye makazi aliyokua akifugwa huko Walkerville kusini mwa Johannesburg.

Chui huyo  alitoroka baada ya uzio kukatwa Jumamosi usiku, vyombo vya habari nchini humo

vimeripoti.Inasemekana alimshambulia mtu. Pia ilimuua mbwa na kumkandamiza mwingine.Mamlaka za utunzaji wa wanyama zimewataka watu kutomsogelea chui huyo  kwa usalama wao, kwani ni hatari.