Jumamosi , 5th Dec , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija,amewataka wananchi waishio pembezoni mwa mito kuacha kutupa taka kwenye mito ili kutunza bahari na kulinda viumbe vilivyomo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija pamoja na wadau mbalimbali wakishiriki zoezi la usafi

Akizungumza wakati ufanyaji wa zoezi la usafi katika fukwe za coco Mkuu wa Wilaya amesema utunzaji wa mazingira unasaidia kulinda afya ambapo amewataka wananchi wote kushiriki katika zoezi la usafi.

Amesema zoezi hilo litaendelea kufanyika ambapo viongozi kuanzia serikali za mitaa watakuwa wakifanya tathmini ili kubaini wale wote wanaokiuka agizo hilo.

Nao baadhi ya wadau mbalimbali wa mazingira wamesema kwa sasa zoezi la ufanyaji usafi ni endelevu ambapo litakuwa likifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.