Jumatatu , 23rd Mei , 2016

Wito umetolewa kwa vijana wa Kitanzania kubadili fikra kuwa maisha mazuri yanapatikana mijini pekee na badala yake wageukie kilimo kwani kilimo kinaonekana kuwanufaisha na kuwainua vijana wengi.

Wito huo umetolewa na msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz alipokuwa akizindua shindano la matumizi ya bidhaa za kilimo hii leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa vijana wengi hawaamini katika kilimo ilihali kunafursa nyingi za kilimo zimeibuka hivi sasa.

Aidha, Diamond amesema kuwa hata kama kijana asiposhiriki katika zoezi la kilimo moja kwa moja anaweza kuwekeza kwenye kilimo kwa kuajiri watu watakaomsaidia kufanya kazi hali ambayo itamfanya atoe ajira kwa vijana wengine na kusaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.