Ijumaa , 11th Apr , 2014

Mkuu wa mkoa wa Kagera nchini Tanzania Kanali mstaafu Phabiani Masawe amewatoa hofu wananchi wa mkoa huo kwa kusema kwamba hali ya usalama imeimarishwa.

Mkuu wa mkoa wa Kagera nchini Tanzania, kanali mstaafu Fabian Masawe

Kauli ya kanali mstaafu Masawe imekuja kufuatia tukio la hivi karibuni la kuingia watu wanaodaiwa kuwa ni askari kutoka nchini Uganda ambapo baadhi ya wananchi mkoani humo walijeruhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kufuatia mkoa huo kuzindua mbio za Mwenge tarehe 2 Mei mwaka huu, Kanali Phabiani amesema wananchi wasiwe na hofu katika kuhudhuria uzinduzi wa mbio hizo, kwa kuwa tayari watu waliohusika na tukio la kuvamia wananchi na kuwajeruhi wameshadhibitiwa.

Amesema katika uzinduzi huo, viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya kutoka nchi za Afrika Mashariki wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo.