
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Muliro
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amebainisha kuwa Mtuhumiwa huyo alikamatwa Novemba 24 mwaka huu maeneo ya Kwembe Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo wakati wa kukamatwa kwake, alitoa bastola yake na kuanza kuwashambulia askari.
Aidha Muliro amebainisha kuwa Mtuhumiwa huyo alikiri kufanya matukio mbalimbali ya uporaji jijini Dar es Salaam, akifafanua kuwa kwa sasa Mtuhumiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kujeruhiwa, kwenye majibizano ya risasi na askari.
Jeshi la Polisi linaendelea kumuombea mtuhumiwa apone haraka ili aendelee na mahojino zaidi, huku likiwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo.