.jpg?itok=FUWcgsV8×tamp=1492532830)
Prof Kitila Mkumbo (Kushoto)
Prof: Kitila Mkumbo ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara katika shirika hilo na kukutana na watendaji wakuu wa DAWASCO pamoja na watendaji wakuu kutoka Mamlaka ya maji safi na taka jijini Dar es salaam DAWASA.
“Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki kwa wananchi”. Alisema Prof. Kitila
Pamoja na hayo amewasii wateja wote wa DAWASCO kutii agizo la Mhe. Rais kwa kulipia huduma wanazozipatiwa ili kuziwesha mamlaka hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Prof: Mkumbo pia amelitaka shirika hilo kukamilisha miradi ya maji katika maeneo ambayo mpaka sasa inaonekana haijakamilika kwa lengo la wananchi kupata maji.
Mtazame hapa kupitia kipindi cha Kurasa