
Daktari Mfawidhi wa kituo hicho Dkt Paschal Kalinga amesema kituo hicho kinahudumia wagonjwa 120 hadi 145 kwa siku hivyo kuwepo kwa changamoto hizo kunapelekea kushindwa kutoa huduma ipasavyo na kuwaomba wadau kujitokeza kusaidia kutatua changamoto hizo.
Kufuatia uwepo wa changamoto hizo Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Misungwi imesema serikali inaendelea kutatua changamoto hizo ambapo Jumatatu vitanda vya wagonjwa vitapelekwa katika kituo hicho.