Jumanne , 10th Jun , 2014

Chama cha Wanasheria cha Tanganyika TLS na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC wametangaza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Juu ya kesi waliyoifungua dhidi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda.

Makamu wa rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) wakili Bi. Flaviana Charles (kushoto).

Akiongea leo jijini Dar-es-Salaam Makamu wa Rais wa chama hicho wakili . Flaviana Charles amesema kuwa, wameridhia uamuzi wa mahakama lakini wameamua kukata rufaa juu ya maneno ya kuwa TLS na LHRC havina uwezo wa kufungua kesi dhidi ya Waziri Mkuu kwa kuwa kauli yake haiwaathiri wao moja kwa moja.

Wakili Flaviana amewataka wanasheria, viongozi na wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana wafanye juhudi za kuhakikisha, utawala wa sheria nchini unafuatwa pasipo kuvunja katiba ili kuleta amani na utulivu pamoja na maendeleo ya nchi.