Ijumaa , 30th Aug , 2019

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa onyo kali kwa vyama vya siasa nchini ambavyo vimetangaza kufanya mikutano ya hadhara kabla ya muda uliopangwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola

Waziri Lugola ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, akisisitiza kuwa, Jeshi la Polisi lipo imara kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu mwakani, hivyo vyama vya siasa vilivyotangaza kuanza kampeni kabla ya muda Jeshi lake litavishughulikia ipasavyo.
 
Pia Lugola amesema Serikali ya Magufuli haiwezi kuchezewa na wanasiasa wanaotaka kuchafua amani ya nchi, hivyo wanaojaribu kumtikisa Rais Mafuguli hawatamuweza.

Pia Waziri Lugola, alipoulizwa kuhusu vituo vya polisi kutotoa dhamana saa 24 kama alivyoelekeza kwa nchi nzima, alishangazwa kama kuna baadhi ya vituo hivyo kuendelea kuvunja maagizo yake, hivyo aliitoa namba yake ya simu ya mkononi na kuwataka wananchi kumpigia endapo watakuwa wanaonewa na askari yeyote wa idara yoyote anayoingoza.

Aidha, Waziri Lugola amepiga marufuku tabia ya Watanzania kuchukua sheria mkononi katika matukio yoyote yanayotokea nchini, amesema kumvamia mharifu na kumpiga ni kosa kisheria pamoja na matukio mengineyo kitendo hicho umemuhukumu.