
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ester Bulaya
Mhe. Bulaya ametoa kauli hiyo leo Juni 7, 2021, bungeni Jijini Dodoma, wakati akiuliza swali kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu ni lini sasa serikali itahakikisha Mahakama ya wilaya hiyo inakuwa na jengo lake kabisa.
"Wilaya ya Bunda haina jengo la Mahakama imepanga kwenye nyumba ya Mzee Wasira kwa muda mrefu, sasa hivi wameamua kupanga kwenye nyumba nyingine, je ni lini wilaya hiyo itakuwa na jengo la Mahakama?"aliuliza Mhe. Bulaya.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geofrey Pinda amesema "Kufikia 2025 sehemu zote ambazo hazina Mahakama za wilaya na makao makuu ya Tarafa zote katika ngazi ya Kata zitakuwa na majengo mapya, tuvumilie tutaendelea kuazima majengo ila 2025 ni mwisho".