Jumanne , 17th Jan , 2023

Makundi ya upinzani nchini Afrika Kusini, chama cha wafanyakazi na wamiliki wa biashara wametishia kuishtaki serikali kufuatia mgao mkali wa umeme nchini humo.

Serikali ya nchi hiyo imepewa  hadi Ijumaa kuimarisha usambazaji wa umeme au kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kukiuka wajibu wake wa kutoa huduma ya umeme umeme.

Imeandikwa  barua ya mahitaji kwa Waziri wa Makampuni ya Umma Pravin Gordhan na afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya huduma za serikali ya Eskom, Andre de Ruyter, barua ikisema serikali inakiuka wajibu wake wa kutoa umeme.

Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa kumekua na Ukataji  wa umeme nchini humo , huku kukiwa na usimamizi mbaya na ufisadi katika kampuni ya serikali ya Eskom

Hivi karibuni nchi imekuwa ikikabiliwa na hadi saa 10 za kukatika kwa umeme kila siku.

Tatizo hilo limemfanya rais kufutilia mbali ziara yake katika kongamano la kiuchumi duniani mjini Davos ili  kufanya mikutano nyumbani na wafanyabiashara na viongozi wa wafanyakazi.