Jumatatu , 22nd Jun , 2020

Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza rasmi kuwa pazia la mchakato wa kuchukua na kurejesha  fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu 2020 utafanyika kuanzia julai mosi, 2020.

ACT-Wazalendo

Akitoa ufanunuzi huo mbele ya wandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ado Shaibu amesema wenye nia ya kugombea nafasi ya Udiwani, Ubunge, Uwakilishi pamoja na Urais bara na visiwani wajitokeze kuanzia hiyo Julai Mosi hadi 13 Julai 2020.

Aidha amesisitiza wagombea wote kuepuka vitendo vya rushwa na kwamba yeyeto atakayejihusisha, chama hakitamvumilia ikiwa ni pamoja na kumchukulia hatua za kinidhamu.

Amesema Viongozi Wakuu wa chama hicho bado wanaendelea na jitihada za kuimarisha uhusiano  baina ya vyama vya upinzani vyenye lengo la kuing'oa CCM madarakani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020.