
Katika taarifa ya Polisi iliyosomwa ndani ya mahakama ya nchi hiyo inaeleza kuwa kesi tatu za matumizi ya bangi zimeshindwa kuendelea kutokana na Panya kula bangi hiyo ambayo ilihifadhiwa kama ushahidi
Jaji wa mahakama ya nchi hiyo Sanjay Chaudhary amesema baadhi ya kesi zimekwama kutokana na polisi kuwalaumu Panya kwa kula bangi waliyohifadhi vituoni
Polisi wanasema hawana utaalamu wa kushughulikia suala hilo kwani panya hao ni wadogo mno huku wakisema njia pekee ya kulinda bangi iliyokamatwa isiliwe na Panya ni kuipiga mnada kwa maabara za utafiti na makampuni ya dawa ili serikali ipate mapato.
Hata hivyo wataalamu wa masuala ya madawa nchini humo wamepinga madai hayo wakisema kwamba wanyama hao hawana uwezo wa kufanya jambo hilo na kama ingetokea basi panya wengi wangekutwa wamefariki katika maeneo hayo