Jumanne , 16th Jun , 2020

Rais Magufuli ametangaza kufungua shule zote zilizokuwa zimebaki kuanzia Juni 29, 2020.

Rais Magufuli

Rais Magufuli ametoa tamko hilo leo Juni 16, wakati akihutubia pamoja na kuhutubia bunge la 11 jijini Dodoma.

“Kutokana na mwendendo wa corona kuendelea kuwa mzuri, corona imepungua sana, naomba nitangaze kuanzia Juni 29, shule zote zilizokuwa zimebaki zifunguliwe, lakini Watanzania waendelee kuchukua tahadhari”, Rais Magufuli.

Aidha Rais ameruhusu shughuli zingine zote ziendelee nchini ikiwemo sherehe mbalimbali kama harusi na mikusanyiko mingine.

Aidha amewashukuru Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, madaktari na watendaji wote wa afya pamoja na watumishi wa dini ambao walikubali kufanya maombi maalumu kwaajili ya kujikinga na Corona.

Tazama Video hapa chini