Jumatano , 11th Jan , 2023

Rais mpya wa Peru Dina Boluarte na mawaziri kadhaa wa nchi hiyo wanachunguzwa kutokana na mapigano ya wiki kadhaa ambayo yamesababisha vifo vya makumi ya watu

Mwendesha mashtaka mkuu wa Peru amesema maafisa hao wanachunguzwa kwa tuhuma za mauaji ya halaiki, mauaji yaliyosababisha madhara makubwa

Ghasia hizo zilizuka baada ya aliyekuwa Rais Pedro Castillo kukamatwa mwezi Desemba mwaka jana kwa kujaribu kulivunja Bunge

Siku ya Jumatatu, watu 17 walikufa katika mapigano kati ya wafuasi wa Castillo na vikosi vya usalama kusini-mashariki mwa Peru huku wengine kadhaa wakijeruhiwa