Ijumaa , 13th Mei , 2022

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibunge amezindua Maabara ya upimaji wa afya ya Udongo na utoaji wa mafunzo kwa wakulima ambapo upimaji huo utamsaidia mkulima kuacha kulima kwa mazoea na kulima kilimo chenye tija 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Maabara hiyo Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema wakulima wa mkoa wa Ruvuma wanategemea sana mvua katika shughuli zao za kilimo hali inayofanya kulima kipindi cha masika tu hivyo baada ya kupima udongo mkoa utagundua maeneo ambayo udongo wake utafaa katika kilimo cha umwagiliaji.

Akielezea zoezi la upimaji litakavyofanyika katika mkoa wa Ruvuma Dr. Mshindo Msola ambaye ni Mkurugenzi wa OCP Afrika amesema mkoa wa Ruvuma watapima afya ya Udongo katika vijiji 100 na kushauri aina ya mbolea itakayofaa katika eneo ambalo limepimwa.

Kwa upande wake Dr. Tulole Busheyeki ambaye ni Mkurugenzi wa  kituo cha taasisi ya utafiti wa kilimo Uyole pamoja na wadau wa kilimo wa mkoani Ruvuma wamesema upimaji wa afya ya udongo utakuwa na faida kubwa kwa wakulima na utawasaidia wakulima kuacha kulima kwa mazoea na kutumia Mbolea bila kujua udongo unakubali mbolea ya aina ipi.