Tutaitisha baraza kujadili kuhusu Zanzibar- Mziray

Ijumaa , 15th Jan , 2016

Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini Peter Kuga Mziray amesema wanajipanga kukutana na kuitisha baraza la mashauriano baina ya vyama vya siasa na Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC wakati wowote visiwani Zanzibar kwa ajili ya majadiliano.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Peter Kuga Mziray.

Mziray amesema hayo kupitia kipindi cha HOT MIX kinaruka EATV kila siku (Jumatatu hadi Ijumaa) saa 12:00 jioni na kuongeza tayari walishatoa muda wa kutosha kwa vyama vya CCM na CUF kutatua tatizo hilo kwa amani na maelewano lakini vimeshindwa kutumia busara kumaliza tatizo hilo.

Aidha Bw. Mziray ameongeza kuwa imewalazimu baraza hilo kuingilia kati suala la utatuzi wa mgogoro huo baada ya kuona mvutano ukizidi bila ya kupatikana suluhu kwa wakati muafaka hivyo watatoa mapendekezo ya kutatua tatizo la mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa baraza hilo la usuluhishi linaundwa na vyama vyote vyenye usajili nchini ambalo litazingatia zaidi maslahi ya taifa kwa ujumla na kukuza demokrasia ya Tanzania Bara na visiwani bila kuleta machafuko