
Kadogosa, ameyasema hayo kwenye misa ya kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi ya ujenzi wa Taifa anayoifanya tangu aingie mamlakani, iliyofanyika Kijiji cha Mwakibuga Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu
"Taifa letu tumetumia (Sh) Trilioni 23.5 Trilioni. Nataka watu ambao msielewe maana yake ni nini, tungetaka kujenga barabara kwa haya mapesa ambayo Mhe Rais (Samia Suluhu Hassan) tungejenga barabara zisizo chini ya kilomita 23,000. Kwa fedha hizi tungesema tunajenga barabara tungejenga mara mbili ya barabara tulizojenga kabla ya uhuru. Kwa hiyo ni uwekezaji mkubwa sana na tunahaki zote za kumuombea Mhe Rais," amesema Kadogosa.
Mapema wakizungumza na waumini wa dini mbalimbali waliohudhuria misa hiyo, Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ngulyati Wilaya ya Bariadi, Padri Andrea Mabula, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony John Mtaka, wamewaomba Watanzania kuendelea kutunza amani ya nchi na kushiriki shughuli za maendeleo.
"Shughuli ya kumheshimisha Rais namna nzuri ni kufanyakazi, kusimamia miradi, fedha anayoileta isimamiwe kwa uaminifu. Kazi za mama Samia Simiyu (Mkoa) hazihitaji tochi. Mnaposema miradi inaendelea kwa nini Simiyu mna miaka tisa, kumbe miradi yenyewe ni pamoja na mradi wa Malampaka (SGR) kwani umesimama?" amesema RC Mtaka.
"Ni kazi ya viongozi wetu kusimamia hiyo amani. Ndiyo maana tunamuombea Rais pamoja na waandamizi wake (viongozi) ili Mwenyezi Mungu awaimarishe katika kuipenda hiyo amani na kuitetea, kuiishi hiyo amani," amesema Paroko Mabula.
"Mhe Rais jamani ndiye anayebeba maono ya Watanzania wote na kuyaweka katika vitendo. Tuna kila sababu ya kumuombea aendelee kuwa mwenye afya njema, ili haya Watanzania wanayoyatarajia basi yaendelee kusimamiwa ipasavyo," amesema RPC Chatanda