Jumanne , 31st Dec , 2019

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, upelelezi wa kesi ya mfanyabishara Khamis Saidy, anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya kumuua na kisha kumchoma moto mke wake Naomi Marijani, tayari umekwishakamilika.

Mfanyabiashara, khamis Saidy aliyemuua mke wake na kumchoma moto

Wakili Wankyo ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ambapo imepigwa kalenda hadi siku ya Januari 7, 2020, itakapotajwa tena.

Mfanyabishara Khamis Saidy, anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni, baada ya kumuua na kisha kumchoma moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake na kisha kuyabeba mabaki ya mwili huo na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.