Alhamisi , 20th Dec , 2018

Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee amesema kuwa vyama vya upinzani vimekuwa vikiungana kipindi ambacho muda unakuwa umeenda na matokeo yake kupelekea kufanya maamuzi ya haraka.

Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee.

Mdee amefunguka kuwa hali hiyo inachangiwa na mapungufu ndani ya vyama hivyo, na kuzidiwa na nguvu kubwa kutoka nje.

"Changamoto ambayo imekuwepo miaka yote tangu mfumo wa vyama vingi uanze ni kwamba kila chama kimekuwa kikifanya kazi peke yake na tumekuwa tukiungana kwa kuchelewa, tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu ndio tumekuwa tunaungana na kukubaliana mambo kadhaa kwa haraka", amesema Mdee.

Mdee amesema kuwa kitu ambacho wanajaribu kukitafuta sasa hivi ni kutengeneza uongozi madhubuti, ili kudhibiti nguvu za nje na kujenga imani miongoni mwao.

Vyama vya Upinzani nchini vimeazimia kuanza kufanya mikutano ya hadhara kwa kile ilichodai kuwa ni kwa mujibu wa haki zao kisheria na kikatiba, hali ambayo inaonekana kuwa tofauti na msimamo wa serikali kuhusu suala hilo.

Vyama hivyo vimeazimia kufanya mikutano ya hadhara kuanzia mwaka 2019 kwa kile ilichodai kuwa ni kwa mujibu wa haki zao kisheria na kikatiba, hali ambayo inaonekana kuwa tofauti na msimamo wa serikali ambayo ilipiga marufuku kwa viongozi wa kisiasa kufanya mikutano ya hadhara isipokuwa kwa wabunge katika majimbo yao husika