Ijumaa , 20th Jan , 2023

Nchi ya Mali imepokea usafirishaji wa ndege za kivita na helikopta kutoka Urusi huku Moscow ikizidisha ushiriki wake nchini humo.

Tangu kuvunja uhusiano wake na Ufaransa, utawala wa kijeshi nchini Mali umekuwa ukimtegemea mshirika wake mpya, ambaye inasemekana amepeleka askari  kutoka kundi la Wagner linalopambana nchini Ukraine, kulingana na vyanzo kadhaa.

Waandishi wa habari wanasema wanajeshi  wa Russia  hawahusiki vilivyo  katika mapambano dhidi ya uasi wa vikundi vya kigaidi, na wanaonekana kujikita katika kupata rasilimali za madini za Mali kwa ajili ya unyonyaji.

Urusi pia imeshutumiwa kwa kujihusisha na taifa jingine la Afrika, Eswatini, ingawa balozi wa Moscow imekanusha  ripoti kwamba inatoa mafunzo kwa maafisa wa usalama.

 Kwa mujibu wa afisa Alexander Surikov alisema ilikuwa tu kutoa ufadhili wa masomo kwa elimu ya kijeshi.