
Balozi Ombeni Sefue
Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom, Balozi Ombeni Sefue amesisitiza kuwa misingi ya uongozi bora aliyoiweka Mwalimu Nyerere inaendelea kuwa mfano mzuri kwa viongozi mbalimbali Afrika.
"Misingi ya uongozi bora kwa matendo ndio imemfanya Mwalimu Nyerere kuwa mfano halisi wa kuigwa kwa viongozi wengi barani Afrika." Amesema Balozi Ombeni Sefue
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro amefafanua kuwa Rais Samia anayaendeleza yale yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa hasa katka kuimarisha mahusiano na mataifa mengine huku Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akimpongeza Rais Samia kwa namna anavyopambana naadui ujinga kwa kuweka msisitizo kwenye elimu nchini.
"Ziara za Rais Samia nchi za jirani baada ya kuingia madarakani zilikuwa ni muhimu sana, na ilibidi afanye vile haraka, na asingefanya vile tusingeeleweka tunasimama wapi baada ya Rais Magufuli kuondoka" amesema Dkt. Asha Rose Migiro, Balozi wa Tanzania Uingereza