
Wakiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo umoja huo umesema walimu hao watapatiwa vitambulisho maalum na watapanda mabasi hayo ya daladala bure kuanzia saa 11:30 asubuhi mpaka saa mbili asubuhi na utaratibu huo utajirudia tena saa tisa alasiri wakiwa wanatoka mashuleni mpaka saa mbili usiku siku za kazi.
Katika hatua nyingine chama cha wafanyakazi madereva nchini Tanzania TADWU kimesema kuna mgogoro mkubwa kati yao na madereva unaotokana na kuchelewa kuchukuliwa hatua ikiwemo za kupatiwa maslahi ya madereva wanayoyadai.
Mwenyekiti wa TADWU Bw. Shabaan Mdemu amesema kwamba ucheleweshaji huo ikiwemo wa kupatiwa mikataba kwa madereva pamoja na stahiki zao wanazozidai muda mrefu kunaweza kusababisha kusitisha huduma kwa madereva jambo ambalo litaleta usumbufu kwa abiria.