Ijumaa , 17th Dec , 2021

Mbunge wa Viti Maalum kundi la NGO's, Neema Lugangira, amesema kuwa bado ipo haja ya kuendelea kuwanyanyua wanawake, kutokana na mfumo uliowekwa wa kwamba kila atakachokifanya mwanamke basi wanaume watamtolea macho kisa tu kafanya kwa ubora kuwazidi wao.

Mbunge wa Viti Maalum kundi la NGO's, Neema Lugangira

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 17, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio na kusema kwamba, hata kwenye mitandao ya kijamii wabunge wanawake wanapitia ukatili mkubwa ikilinganishwa na wanaume.

"Bado kuna 'gape' kubwa sana kati ya mwanaume na mwanamke, hata kwenye kugombea kwenye nafasi za uongozi, hata kwenye mitandao ya kijamii kunakuwa na ukatili mkubwa sana wa kijinsia kwetu sisi wabunge wanawake tofauti na wanaume," amesema Mbunge Neema