Jumatatu , 13th Sep , 2021

Raia 16 wa Ethiopia wakiwemo watoto 11 wamekamatwa na Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuingia nchini bila kufuata taratibu za kisheria, huku jeshi hilo likimshikilia Yohana Adam Mkazi wa Kasumulu wilayani Kyela kwa tuhuma za kuwasafirisha wahamiaji hao kuwapeleka nchi jirani ya Malawi.

Wahamiaji haramu waliokamatwa mkoani Mbeya

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema watu hao wamekamatwa katika Kijiji cha Namba One kilichopo Kata ya Isongole wilayani Rungwe.

Aidha, Matei amewataka madereva wa magari nchini hasa vijana kuacha kufanya kazi hiyo ya kuwasafirisha wahamiaji haramu hao akidai kuwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria na kwamba adhabu yake ni kutaifishwa kwa gari na mhusika kutozwa faini kubwa.