Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa wa Mwanza, ambapo pamoja na mambo mengine kilijadili namna ya kukabiliana na upungufu wa walimu vijijini.
Amesema uwekwe utaratibu kila anayeomba ajira ya Ualimu aingie mkataba na serikali kwamba kwa miaka kumi atakaa katika kituo cha kazi bila kuhama na kuweka bayana kuwa hii itapunguza uhaba wa walimu vijijini.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema ili kuboresha elimu mashuleni ni lazima kuweka utaratibu wa kufanya kwa wazazi wanaowakingia vifua wanaume wanaowapa mimba wanafunzi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Mwanza , Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali na watoa huduma mbalimbali za kijamii.