Alhamisi , 2nd Feb , 2023

Mamlaka nchini Zambia imepitisha sheria inayokataza watembea kwa miguu kuvuka barabara wakiwa wamevaa  earphones  au kuzungumza kwa simu ya mkononi.

Mtu anayekiuka kanuni hii anatenda kosa na anawajibika, kwa kutiwa hatiani, kwa faini isiyozidi kwacha 1,000  sawa na karibia shilingi 40,000 za kitanzania  kwa mujibu wa kifungu cha sheria mpya.

Mtembea kwa miguu lazima asubiri taa za barabarani zigeuke nyekundu kwa magari kusimama, kabla ya kuvuka barabara kwenye makutano ambayo yanadhibitiwa na taa za barabarani, inasema sheria hiyo.

Frederick Mubanga, msemaji wa chombo hicho kinachoshughulikia usalama barabarani, anasema sheria hiyo inalenga kudhibiti ajali za barabarani.

Amesema kwamba   zaidi ya asilimia 50 ya watu wanaofariki kutokana na ajali za barabarani ni watembea kwa miguu. Na mara nyingi, watembea kwa miguu huenda hawakutumia barabara kwa usahihi.

Bw Mubanga alisema polisi watatafuta hati za kukamatwa dhidi ya wahalifu ambao hawalipi faini hiyo.