
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa wakala hiyo mkoani Morogoro kwa kuzingatia ni chombo muhimu kwa watumishi kukutana kujadili masuala muhimu ya taasisi yao na kufanya maamuzi.
Waziri Mhagama alieleza ipo haja ya kila mtendaji katika Taasisi hiyo kuona umuhimu wa kutekeleza majukumu yake kwa weledi kwa kuzingatia mchango unaotolewa na OSHA katika kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati kwa kuzingatia majukumu yake ya msingi.
“Jitihada za OSHA katika kutekeleza majukumu yake zina mchango mkubwa kuendeleza uchumi wa viwanda na kuboresha mazingira ya biashara na Uwekezaji nchini na ni ishara ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, ya kukuza viwanda” alisema Waziri Mhagama.
Aliongezea kuwa, kuwe na jitihada za makusudi za kila mfanyakazi kutambua umuhimu wa kubadili mitazamo hasa kiutendaji kwa kuondokana na mazoea na kuendana na kasi ya awamu hii.