Alhamisi , 17th Nov , 2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Mifugo a Uvuvi, kuandaa mikutano ya mara kwa mara na wadau wa uvuvi ili kujadili changamoto zilizopo katika sekta hiyo na kuzipatia ufumbuzi kufuatia mazao ya uvuvi kutajwa kupungua katika ziwa victoria.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Hayo ameyabainisha kwenye kikao maalum kilichowakutanisha viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa uvuvi wa mikoa mitano ya kanda ya ziwa lengo lake ni kujadili ulinzi, uzalishaji na usimamizi wa samaki nchini, hali iliyopelekea Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambae amemuwakilisha Waziri Mkuu Majaliwa kuagiza vikao vya mara kwa mara vinakuwepo ili kuhakikisha samaki wnaendelea kuzaliana.

"Naiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inaandaa mikutano ya mara kwa mara na wadau wa uvuvi ili kujua changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka pia ihakikishe inaendelea kutoa elimu kwa wavuvi hao kuhusu kupambana na uvuvi haramu ili samaki wetu kwenye ziwa victoria wasipungue," amesema Waziri Mkuu

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima, amesema kwa mwaka 2021 mkoa huo umekusanya shilingi bilioni 3.42 zilizotokana na ushuru na leseni za uvuvi na bado jitihada za kuongeza makusanyo zinaendelea.