Alhamisi , 6th Oct , 2022

Wizara ya Afya imeombwa kuangalia upya swala la utoaji huduma za afya bure kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano hasa wale wanaolelewa katika vituo vya watoto yatima na waliopo kwenye makundi maalumu

Hii ni kutokana na kuwepo kwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza ikiwemo kutokupatikana na kwa baadhi ya huduma za afya kwa watoto hao hivyo vituo hivyo kulazimika kulipia gharama za matibabu kwa watoto hao.

Ombi hilo liimetolewa na mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Mgolole sista Maria Anitha wakati wa hafla ya kusherekea sikukuu ya Mt Vicent Wa Paulo ambapo amesema licha ya serikali kutangaza uoaji wa huduma ya afya bure kwa watoto chini ya miaka mitano katika hospitali za serikali bado hali imekuwa tofauti kwasababu baadhi ya huduma hazipatikani na kulazimika kutoa gharama katika kuwahudumia watoto hao

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mtendaji mkuu wa wakala wa mbegu za kilimo nchini ASA Dkt Sophia Kashenge amesema kufuatia ongezeko la idadi ya watoto wenye uhitaji maalum linalosababishwa na vifo vya wazazi kanisa katoliki kuangalia namna bora ya kuanzisha vituo vya kusaidia watu wazima wanaokabiliwa na changamoto hiyo

Aidha katika maadhimisho hayo wakala wa mbegu ASA imetoa msaada wa maguni kumi ya mpunga yenye shilingi milioni moja pamoja na mafuta ya alizeti lita arobaini.