Jumapili , 22nd Dec , 2019

Saa chache kabla ya timu ya Lipuli kucheza mchezo wake dhidi ya Dar City ya Dar es salaam kwenye michuano ya Kombe la FA ambapo Lipuli ilishinda kwa mabao manne 4 - 0. Msanii wa Muziki Alikiba alifanya mazoezi na wachezaji wa Lipuli.

Alikiba

Alikiba alifanya zoezi na wachezaji wa Lipuli ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa Tamasha lake la Alikiba Unforgetable Tour, ambayo ilifanyika uzikuwa kuamkia bna kushuhudia mamia ya watu kumiminika kwenye Tamasha hilo.

Katika Tamasha hilo Alikiba alimpandisha Mkuu wa Wila ya Iringa Mjini Richard Kasesela ambaye kama kawaida yake alitumbuiza kwenye majukwa ya burudani.