Ben Pol awataja wanao mmendea mchumba wake

Alhamisi , 6th Jun , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ben Pol, ameweka wazi kuwa kuna wasanii huwa wanamtumia meseji mchumba wake Anerlisa, na mara nyingi huwa anaziona.

Akizungumzia hilo Ben Pol amesema kuwa ameshawahi kukuta meseji za watu mbali mbali wakiwemo wasanii Shetta, Harmonize, na msanii wa Kenya Kaligraph Jones, lakini amekuwa hazitilii maanani.

“Nawaona, Shetta, Kaligraph, naona 'blue ticks' lakini sishangai  kwa sababu ni msichana mrembo, na ukikaa naye kama hivi ndio unaona urembo wake”, amesema Ben Pol.

Ben Pol kwa sasa yuko kwenye mahusiano rasmi na Anerlisa baada ya kumvisha pete ya uchumba, jambo ambalo mwenyewe anasema ni kitu kikubwa kwenye maisha yake.