FA azungumzia kuhusu urafiki na kugombana na AY

Jumatano , 7th Aug , 2019

MwanaHipHop mkongwe hapa nchini Tanzania Mwana Fa, amefunguka suala la kugombana na rafiki yake na msanii mwenzake wa muda mrefu AY.

Mwana Fa amesimulia hayo leo kupitia EATV & EA Radio Digital na kusema kuwa huwa wanagombana sana na AY.

"Tunapishana, kugombana na kubishana kila siku ila tunalala tukiamka tunaangalia mambo mengine, vitu hivyo vipo na vinatokea ila huwa tunarudi nyuma kuangalia kitu gani kilichotufanya tunagombana sio kulipiziana visasi."

Urafiki wa Mwana Fa na AY umedumu kwa miaka 17 na ulianza mwaka 2002, katika kundi la East Cost Team walipokuwa na wasanii wengine wakiwemo GK.

Aidha msanii huyo amezungumzia suala lake la kuingia katika biashara na kusema, yeye sio wa kwanza kufanya hivyo hata Jay Z, P.Diddy na Rihanna wanafanya.

Pia amesema pesa inayofanya kuonekana kupata maendeleo kwa wasanii haitoki kwenye show na muziki peke yake bali na uwekezaji mwingine.