Jumatano , 19th Jun , 2019

Familia ya mzazi mwenzake marehemu Agnes Gerald (Masogange), imeweka wazi kuwa mpaka sasa haijapokea pesa yoyote iliyochangwa kutoka kwa wasanii, ambayo waliahidiwa kuwa watapewa.

Wakizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, dada wa mzazi mwenzake Agnes, anayejulikana kwa jina la Sania, amesema kuwa mpaka sasa hawajapesa pesa yoyote, hata ile ahadi ya kumkatia mtoto bima ya afya haijafanyika.

Akiendelea kueleza hayo Sania amesema kwamba yalipotoka majibu kuwa mtoto wao amefaulu, mmiliki wa shule ya St. Patrick alijitolea kumsomesha mtoto huyo, pamoja na kugharamia gharama zote atakapokuwa shuleni, jambo ambalo linafanyika mpaka sasa.

Hata hivyo familia hiyo imesema haikutaka kwenda kuulizia juu ya pesa hiyo, kwani hawataki kuonekana kama wamezitolea macho ili wazitumie kinyume na utaratibu uliowekwa.

Sikiliza mahojiano yao hapa kati ya Big Chawa na familia ya Masogange.