Gelly wa Rhymes kulelewa na jimama Arusha

Jumanne , 11th Feb , 2020

Msanii Gelly Wa Rhymes amefunguka na kusema yeye ni bishoo lakini ni mpambanaji na watu wasimchukulie poa, kama analelewa na mwanamke ambaye amembadilisha dini na kumuhamisha Jiji.

Picha ya msanii Gelly Wa Rhymes

Gelly Wa Rhymes ameeleza hayo alipodakwa na kamera za EATV & EA Radio Digital, ambapo amesema Dar es Salaam ndipo wanaume wanaongoza kulelewa na wanawake ila sio Arusha  anapoishi kwa sasa.

"Watu waniangalie vizuri aisee mimi ni bishoo, nahangaika,  mpambanaji na sikai kizembe, halafu ule Mkoa wa Arusha watu hawaishi hivyo labda huku Dar ndiyo vijana wanalelewa, watu wa kule wamenifundisha maisha ya kukaza maisha yangu ndiyo yapo hivo" amesema Gelly Wa Rhymes.

Aidha ameongeza kusema watu watakuwa wanafeli endapo watamchukulia kama mtoto wa mama asiyeweza kazi.