Kundi la Muziki la Jambo Squad maarufu kama Mamong'oo
Akiongea na Enews Mmoja wa Wasanii wa kundi hilo Chalii Mtoto wa Bibi Nigger amesema wimbo wao huo wa Digidigi utazungumzia sana ishu za ujangili kwa kutoweka kwa wanyama kama vile Tembo, Twiga na wengineo.
Chalii mtoto wa bibi amefunguka zaidi kwa kusema mwaka huu wamepanga kuachia hits baada ya hits na sasa watakuja kwa mtindo wa kuachia video na audio kwa pamoja ili kuonyesha wamedhamiria kulikamata game tena.