Jumatatu , 7th Jun , 2021

Mwimbaji Mariah Carey ameripotiwa kuwa na ugomvi na Rapper na nguli wa muziki Jay Z, na kupelekea kuachana na kampuni yake ya usimamizi yaRoc Nation huku ikielezwa kuwa Carey alitaka kujua juu ya mstakabali juu ya kazi yake kwahapo baadae.

Msanii Mariah Carey

Msuguano mkali kati ya wasanii hawa uliotokea kwenye mkutanowao hivi karibuni ambapo inaripoti Carey amekatisha mahusiano yake yakibiashara na rappper Jay Z, ikiwa ni miaka mitatu na nusu tu tangu ku-signdili na kampuni yake ya usimamizi ya Roc Nation mwaka 2017.

Picha ya pamoja Mariah Carey na Jay-Z

Taarifa zinasema Carey atajiondoa rasmi Roc Nation ndani ya wiki chache kuanzia sasa, ingawa amekanusha kuwa palikuwa na ugomvi mkubwa na rafiki yake huyo wa muda mrefu Jay Z.