Mkasa aliokutana nao Madee akiwa Mahabusu

Alhamisi , 8th Aug , 2019

Rais wa Manzese na Boss wa lebo ya 'MMB' Madee Seneda, leo amekumbuka tukio ambalo limewahi kumtokea miaka mitatu iliyopita baada ya kukamatwa na Polisi.

Msanii Madee (aliyefungwa pingu).

Madee amepost picha kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, ikimuonyesha amefungwa pingu huku ameshikiliwa na polisi na amesema,

"Hiyo picha ni ya muda, sikuwahi kufugwaga pingu hiyo ndiyo mara ya kwanza. Ilikuwa siku kama ya leo (Agosti 7), kuna mtu alinipora simu yangu, mimi nikachukua hatua mkononi ya kumpiga hadi akapelekwa hospitali na mimi nikakamatwa na kuwekwa jela siku mbili".

Pia Madee ameongeza kwa kusema kuwa, baada ya hapo alipewa dhamana na alihukumiwa kifungo cha nje pia alijifunza vitu alivyokutana navyo gerezani ambavyo ni watu wengi waliopo jela wanakamatwa kwa makosa madogo madogo.