Msanii atangaza kuwa Single, kumtaka Vanessa Mdee

Jumanne , 10th Sep , 2019

Msanii Bright ametangaza kuwa 'single' kutokuwa na mahusiano na mwanamke yeyote huku akimsubiria Vanessa Mdee.

Bright na Vanessa Mdee

Bright Music ameileza EATV & EA Radio Digital sababu za kuwa single ni,

"Siko kabisa katika mahusiano  nawaangalia wenye maendeleo, wanawake hawawezi kuwa na 'lofa' lazima uwe na mchele 'pesa' pia uangalie hali yako".

Bright ameendelea kusema alikuwa  kwenye mahusiano ila umaarufu umesababisha  kuna vitu vingi vinatokea, wengi aliokuwa nao waliangalia nafasi yake na hakukuwa na mahaba.

Aidha Bright Music amesema kitu anachovutiwa kwa Vanessa Mdee ni mwanamke mzuri ambaye kila Mwanaume rijali lazima amuelewe na hisia zake zipo kwa Vanessa anampenda na anamkubali.

Bright ameendelea kusema kuwa jambo la kumpata Vanessa Mdee linaweza likawa hivi karibuni waombe uzima na kwa mahaba ambayo atampa atamtuliza mwenyewe.