Msanii wa Bongofleva afiwa na mama yake

Jumatatu , 29th Jun , 2020

Msanii wa BongoFleva kutokea kundi la Wakali Kwanza Makamua amefiwa na mama yake leo hii Juni 29, na msiba upo nyumbani kwao Tabata Kisukulu ambapo anatarajiwa kuzikwa siku ya Ijumaa au Jumamosi.

Msanii wa BongoFleva Makamua

Akizungumza na mtangazaji JR Junior msanii Makamua amesema chanzo cha kifo mama yake ni matatizo ya Moyo na umauti ulimkuta baada ya kudondoka ghafla.

"Mama alikuwa na imani sana ya dini, kuna muda alikua akifanyiwa maombi basi anaamini Mungu atamponya na imani yake ilipelekea akaacha kutumia dawa za kutuliza presha jambo lililopelekea moyo wake ukawa unaongezeka ukubwa kila kukicha

Aidha Makamua ameongeza kusema "Umauti umemkuta baada ya kudondoka ghafla na alipopelekwa hospitali madaktari waliamuru afanyiwe operationbaada ya vipimo, lakini walipomueka kwenye mashine ya kupumulia ubongo wake ulisoma sifuri kitu kilichoashiria alikua ameshafariki kabla ya kupatiwa huduma