Jumatano , 2nd Jun , 2021

The African Princess, Nandy ametangaza kuachia Extended Play (EP) inayoitwa 'Taste' siku ya alhamisi (kesho)  ikiwa ni ya pili ndani ya nusu ya kwanza ya mwaka huu.

Picha ya Msanii Nandy

Nandy bado hayaweka wazi orodha na idadi ya nyimbo zitakazobeba EP hiyo wala wasanii walioshirikishwa.

Ikumbukwe mwezi Machi mwaka huu msanii huyo aliachia EP ya nyimbo 5 ambazo zilikuwa za mahadhi ya Dini na iliitwa 'Wanibariki'.